
Kwa wajukuu wangu wapendwa —
Hadithi hii, urithi kutoka kwa nyanya yenu mkubwa wa zamani, na iwe taa itakayowaangazia njia. Kila mnapoisoma, mkumbuke hekima inayopatikana katika hadithi za kawaida, na methali ya zamani isemayo: “Mtaka vyote hukosa vyote.”
Tembeeni njia yenu kwa ujasiri, chagueni kwa moyo wa wazi, na zibebeni hadithi za familia yetu kama hazina mioyoni mwenu mnapoandika hadithi zenu wenyewe.
Kwa upendo wangu wote,
Nana


Kama ilivyo desturi, jioni moja Nyanya aliketi kwenye mkeka nje ya kibanda cha nyasi. Wajukuu wake walijikusanya karibu naye, wakingoja kwa hamu hadithi ya usiku huo.”
Kwenye bonde lililo chini ya mahali tunapoishi, waliishi fisi wengi. Lakini kulikuwa na mmoja mlafi kupita wote. Tumbo lake lilikuwa limejaa kila mara, lakini tamaa yake haikukoma.
Siku moja asubuhi, fisi huyo aliamka na njaa kali sana. Akaanza kutafuta chakula, akipekua ardhini kwa pua yake.”
Alitembea mbali akafika mahali njia iligawanyika mara mbili. “Fisi, akavuta harufu nzuri ya nyama choma kule kijijini upande wa kushoto. Upande wa kulia, alihisi harufu ya mbuzi.
Gafla, fisi alimwona sungura mnene akiruka mbele yake kichakani. Sungura aliganda kwa hofu. Fisi angemkamata na kumla. Lakini tamaa na kusitasita ilimshika fisi. Fisi aliramba midomo yake akiwaza: “Kwa nini nikubali sungura mdogo? Si ni bora nipate kitu kikubwa zaidi?”
Akamwachia sungura na akaendelea na mipango yake. Akaweka mguu mmoja upande wa kushoto na mguu mwingine upande wa kulia na kuanza kutembea, akipanua miguu zaidi na zaidi.”
- Full access to our public library
- Save favorite books
- Interact with authors
Mimi ni Janerose Ngiri, na hadithi hii ya fisi ni mojawapo ya hadithi nyingi nilizosimuliwa na Nyanya yangu nikiwa mtoto mdogo.
Hadithi hii ilinifundisha kuhusu uaminifu, unyenyekevu, na ukarimu.
Ni furaha yangu kushiriki hekima hii ya utamaduni wetu na kuendeleza roho ya usimulizi kwa kizazi kijacho.

- < BEGINNING
- END >
-
DOWNLOAD
-
LIKE
-
COMMENT()
-
SHARE
-
SAVE
-
BUY THIS BOOK
(from $2.99+) -
BUY THIS BOOK
(from $2.99+) - DOWNLOAD
- LIKE
- COMMENT ()
- SHARE
- SAVE
- Report
-
BUY
-
LIKE
-
COMMENT()
-
SHARE
- Excessive Violence
- Harassment
- Offensive Pictures
- Spelling & Grammar Errors
- Unfinished
- Other Problem

COMMENTS
Click 'X' to report any negative comments. Thanks!